Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Vyama vya Siasa ambavyo vinatarajia kushirikiana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu bila kufuata Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyoainishwa kwenye Kifungu Na.11 (a) cha Sheria hiyo vitakuwa vimevunja sheria.
Serikali inawaonya Wanasiasa kuacha propaganda za kupindisha ukweli na kutoa tafsiri potofu kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2018 kwa lengo la kuuhadaa umma kukataa muswada bali watumie fursa hii baada ya kuusoma , kutoa maoni yao stahiki kwa lengo la kuuboresha
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi anawataarifu wajumbe wote wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa kikao cha Baraza la Vyama vya siasa kilichokuwa kimepangwa kufanyika tarehe 21 na 22 Desemba, 2018 mjini Zanzibar, kimeahirishwa.
Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kimefanyika leo Disemba 4, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Haruna Suleman amesema kuwa Suala la kusimamia vyama vya siasa nchini linahitaji umakini na usimamizi wa hali ya juu ikiwa ni njia bora ya kukuza democrasia na utawala bora nchini.
Maafisa wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wanaojiandaa kushiriki katika uangalizi wa kampeni za uchaguzi unaotegemea kufanyika Decemba 2 mwaka huu, wameaswa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ili kujikita katika kuhudumia Vyama vyote kwa usawa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa mashirikiano kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania ili Ofisi hiyo iweze kutekeleza vyema majukumu yake katika kuimarisha demokrasia nchini.
Viongozi wa kitaifa wa vyama vya Siasa nchini wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa maslahi mapana ya taifa kuepuka kuanzisha vyama kwa maslahi binafsi.