Usajili wa Vyama
- Tunasajili chama cha siasa kinachokidhi vigezo vya usajili kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992. Pia tunafuta chama cha siasa chenye usajili wa muda au usajili wa kudumu ambacho kwa mujibu wa sheria kimepoteza sifa ya usajili.
- Kifungu kidogo (1) cha (20) cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 kinamtambua Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa ndio mwenye mamlaka kisheria ambaye anaweza kusajili na kufuta usajili wa chama chochote cha siasa na kifungu hicho kinatoa mwongozo kuwa uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kusajili au kufuta chama cha siasa ndio uamuzi wa mwisho na hauwezi kukatiwa rufaa.