• English
  • Staff Mail
  • Maswali
  • Wasiliana Nasi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

  • Kuhusu sisi
    • Mamlaka
    • Dira
    • Majukumu
    • Muundo
    • Uongozi
    • Historia
  • Shughuli za Ofisi
    • Usajili wa Vyama
    • Uratibu wa Vyama
    • Ufuatiliaji wa Vyama
    • Gharama za Uchaguzi
    • Ruzuku ya Vyama
    • Utatuzi wa Migogoro
    • Taarifa za Vyama vya Siasa
  • Vyama vya Siasa
    • Usajili wa Kudumu
    • Usajili wa Muda
    • Orodha ya Vyama Vya Siasa
    • Baraza la Vyama
  • Sheria na Machapisho
    • Katiba
    • Sera
    • Sheria
    • Kanuni
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Fomu EE
    • Fomu PP
    • Fomu za Fedha
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Taarifa kwa Umma
  • Matangazo
    • Mikutano
    • Warsha
    • Nafasi za kazi
    • Zabuni
  • Ziara
    • Taratibu za Ziara
    • Fomu ya Maombi
    • Utimilifu na Makatazo
    • Maoni ya Watembeleaji

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa mashirikiano kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania ili Ofisi hiyo iweze kutekeleza vyema majukumu yake katika kuimarisha demokrasia nchini.

Dk. Shein aliyasema hayo leo Septemba 25, 2015 alipokuwa na mazungumzo na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Mhe. Mohammed Ali Ahmed aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha kwa Rais akiwa amefuatana na Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Mhe.Jaji Francis Mutungi.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua umuhimu wa Ofisi hiyo pamoja na uongozi wake kwa Taifa, hivyo kuna kila sababu ya kutoa ushirikiano wake kwa lengo la kuimarisha demokrasia.

Dk. Shein alimpongeza Naibu Msajili huyo wa Vyama vya siasa kwa kuteuliwa nafasi hiyo na kueleza matumaini yake makubwa ya utendaji kazi wa kiongozi huyo.

Aidha, Rais Dk. Shein alimuhakikishia kiongozi huyo kwamba kwa upande wa Zanzibar atapewa kila aina ya msaada na mashirikiano ili aweze kufanikisha kazi zake vyema hasa ikizingatiwa kuwa ofisi yake ipo hapa Zanzibar.

Nae Jaji Francis Mutungi aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Shein kwa mashirikiano makubwa inayoyapata Ofisi yake hatua ambayo imeweza kusaidia kufanikisha vyema kazi za Ofisi hiyo.

Mapema Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mohammed Ali Ahmed alitoa shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo ambao aliahidi kuutumikia vyema.

Naibu Msajili huyo ameahidi kutekeleza vyema majukumu yake ya kazi kwa kusimamia vyema sheria za vyama vya siasa nchini huku akieleza kuwa atahakikisha anatekeleza ipasavyo sheria hizo kwa lengo la kuwatumikia wananchi ili waweze kupata maendeleo sambamba na kuimarisha amani, utulivu, umoja na mshikamano mkubwa uliopo nchini.

Rais Dk. John Magufuli alimteua Mohammed Ali Ahmed tarehe 20 Juni 2018 ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mwanasheria na mtafiti katika Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar ambaye amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Rajab Baraka Juma ambaye amestaafu.

Habari

  • ZINGATIENI SHERIA, KATIBA NA KANUNI YA VYAMA VYENU - MUTUNGI.
    tokea mwezi 1
  • Political Parties Council Urges Ethical Campaigning, Applauds Government’s Gender Initiatives
    tokea miezi 3
  • Msajili Aipongeza CHADEMA kwa Kuonesha Ukomavu wa Demokrasia Nchini
    tokea miezi 5
  • Tanzia
    tokea miezi 6

Nifanyaje...

  • Kusajili Chama cha Siasa?

Machapisho

  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Msimamo wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya CHADEMA
  • KANUNI ZA KURATIBU MIKUTANO YA HADHARA YA VYAMA VYA SIASA YA MWAKA 2023
  • KANUNI ZA KURATIBU MIKUTANO YA HADHARA YA VYAMA VYA SIASA YA MWAKA 2023
  • THE POLITICAL PARTIES AFFAIRS LAWS (AMENDMENT) ACT, 2024
  • ORODHA YA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA 2025

Wasiliana Nasi

  • S.L.P : S.L.P 2851 Dodoma
  • Simu : +255 26 23322500
  • Nukushi : +255 26 2323525
  • Barua Pepe : info@orpp.go.tz
  • Website :https://www.orpp.go.tz

Kurasa za Karibu

  • eOffice
  • Video Mpya
  • Staff Mail
  • Huduma Zetu
  • Vyama Vya Siasa

Tovuti Mashuhuri

  • e-Mrejesho
  • Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Bunge la Tanzania
  • Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tume ya Uchaguzi

Mitandao ya Kijamii

© 2017 Office of Registrar of Political Parties - All Rights Reserved

  • Ramani Ya Tovuti
  • Sera YA Faragha
  • Angalizo