Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, Chama cha siasa ni kundi wa watu wenye lengo la kuunda Serikali kupitia uchaguzi halali.
Ndio, kuna hatua mbili. Usajili wa muda na usajili wa kudumu.
• Wanzilishi wawili watawasilisha maombi ya usajili wa muda kwa kujaza fomu
maalumu wakiambatanisha na katiba na kanuni za chama kitarajiwa.
• Chama tarajiwa kinatakiwa kutoa uhuru wa mtanzania yoyote kuweza
kujiunga bila kuwa na ubaguzi wowote wa kijinsia,kidini, kiitikadi n.k
• Kulipa ada ya maombi ya usajili ya shilingi 25,000.
• Usajili wa muda utadumu kwa muda wa siku 180, ndani ya muda huo,
chama kitatakiwa kutafuta wanachama wasiopungua 2000 ( 200 kwa kila
mkoa) katika mikoa 10, mikoa miwili kati ya hiyo ni lazima iwe Tanzania Zanzibar na mkoa
mmoja kati ya hiyo miwili, uwe Pemba.
• Kutimiza masharti ya usajili wa muda yaliyopo kwenye sheria
• Baada ya kupata wanachama 2000 ndani ya siku 180, Waanzilishi watawasilisha
maombi ya usajili wa kudumu kwa kujaza fomu maalumu.
• Kulipa ada ya usajili wa kudumu ya shilingi 50,000.
• Chama kiwe kimepata Ofisi ya Makao makuu na anuani ya posta kwa ajili ya
mawasiliano rasmi na kuchagua viongozi wa kitaifa.
• Chama kiwe kimetimiza masharti yote ya kupata usajili wa kudumu yaliyopo
kwenye sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho 2015.
Ndio. Chama cha siasa kinaweza kufutwa iwapo chama hicho kitakiuka masharti ya usajili yaliyopo kwenye Sheria au endapo kitakiuka kifungu chochote cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992
Ndio. Msajili atakitaarifa chama husika nia ya kukifuta kwa maandishi akieleza mapungufu aliyoyabaini.
Endapo chama cha siasa kitawasilisha utetezi, Msajili atamutaarifu kwa maandishi Waziri anayeshughulikia mambo ya siasa nia yake ya kutaka kufuta usajili wa chama hicho akiambatanisha na maelezo ya utetezi yaliyotolewa na chama hicho. Kisha Msajili anakitaarifu chama kufutwa kwa usajili kwa fomu maalumu endapo hajaridhika na utetezi wa chama au chama hakijawasilisha utetezi.
Kwa mujibu wa sheria ya nyama vya siasa, Msajili wa Vyama vya siasa ndio mwenye maamuzi ya mwisho kuhusu kukifutia chama usajili wake.
Kuna vyama 19 ambavyo vimesajiliwa venye usajili wa kudumu na chama kimoja chenye usajili wa muda.
Bonyeza hapa kuvifahamu