Rais Samia Awapa Kongole Kikosi Kazi, Aahidi Kufanyiwa Kazi Mapendekezo
Na: Mwandishi Wetu – ORPP
Rais Samia amekipongeza Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini kwa kazi nzuri walioifanya ya kuchambua maoni ya wadau kwa kipindi cha miezi 10.
Pongezi hizo zimetolewa leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea ripoti ya mwisho ya kikosi hicho iliwasilishwa na mwenyekiti wa Kikosi kazi hicho Profesa Rwekaza Mkandala
“Wakati nawapa hii kazi sikujua leo itafika mnikabidhi kitu kilichofanyiwa kazivizuri hivi, kwa hiyo namshukuru Mungu lakini nakushukuruni nanyi na wote mliosaidiana nao katika kazi hii,” alisema Rais Samia.
“lakini la pili niwapongeze kwamba kwa muundo wenu watu kutoka sekta mbalimbali, imani mbalimbali za kisiasa, vyombo vya ulinzi, NGO, vyombo vya habari lakini mmeweza kujipanga na kufanyakazi mkazalisha kitu kizuri ambacho leo mmewasilisha, hongereni sana”.
Rais Samia amesema kuwa pamoja na kuwa kazi hii ilikuwa ngumu lakini kikosi kazi kimefanikiwa kukamilisha kazi hii ndini ya kipindi cha miezi kumi licha ya kwamba wangeweza kwend hadi zaidi yam waka mmoja kutoka na uzito wake.
Aidha katika pongezi hizo Rais Samia akusita kumshukuru Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi kwa kutekeleza wajibu wake katika kuhakikisha anaratibu vyema shughuli za kikosi kazi hicho katika kutimiza majukumu yao.
“Katika shukrani nisisahau Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, wakiongozwa na Jaji Mutungi, Jaji Mutungi saa zingine ananipigia simu usiku we mama wee hii kazi uliyonipa nimekwama hapa na hapa, umeaminiwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa nenda na kazi yako, ukikwama fedha niambie lakini mengine fanya kazi yako, kwa hiyo nakushukuru umefanya kazi yako na mmefikia pazuri”, alisema Rais Samia.
Katika hatua nyingine Rais Samia amesema kuwa Serikali imepokea ripoti ya kikosi kazi ambapo Serikali inajipanga kupitia mapendekezo hayo kupitia vikosi kadhaa vitakavyongalia mambo kadhaa yanayohitaji wataalamu hususan yanayohusu sheria.
Amesema kuwa Kikosi kazi kimetoa mambo mazuri ambayo serikali kupitia wataalam wake kwa kushirikiana na baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi watakaopendekezwa wafanya mapitio ya mapendekezo hayo na kuja na namna bora zaidi ya utekelezaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demeokrasia ya vyama vingi vya siasa, Prof. Rwekaza Mkandara akiwasilisha taarifa ya ripoti yao ametumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Ally Mwinyi kwa juhudi zao za za kuwaletea watanzania na wanzanibar maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hususan kuboresha demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
Prof. Mukandala amesema kuwa Kikosi kazi hicho kilizinduliwa rasmi mnamo tarehe tarehe 11 Januari 2022 na mpaka sasa kimefanya kazi zifuatazo: kupitia hadidu za rejea, kuchambua hotuba za kufungua na kufunga mkutan...