KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA CHA TAREHE 21 NA 22 DESEMBA, 2018 KIMEAHIRISHWA
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi anawataarifu wajumbe wote wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa kikao cha Baraza la Vyama vya siasa kilichokuwa kimepangwa kufanyika tarehe 21 na 22 Desemba, 2018 mjini Zanzibar, kimeahirishwa. Sababu kuu ya kuahirisha kikao hicho ni kutokana na kuwepo kwa zoezi la uteuzi wa wagombea siku ya tarehe 20 Desemba, 2018 katika Jimbo la Temeke Dar-es Salaam na Kata 48 zilizopo katika maeneo ya Wilaya mbalimbali za Tanzania Bara.
“Kwa mujibu wa Kanuni ya 16(4) ya Kanuni za Baraza la Vyama vya Siasa, nimeshauriana na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa na tumeamua kuahirisha kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa mpaka baada ya uchaguzi mdogo wa tarehe 19 Januari, 2018, ili kuwezesha Vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mdogo wa tarehe 19 Januari, 2018” ikisema sehemu ya taarifa hiyo.
Mhe. Jaji Mutungi pia ameomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na kuahirishwa kwa kikao hicho.