Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa mashirikiano kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania ili Ofisi hiyo iweze kutekeleza vyema majukumu yake katika kuimarisha demokrasia nchini.
Viongozi wa kitaifa wa vyama vya Siasa nchini wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa maslahi mapana ya taifa kuepuka kuanzisha vyama kwa maslahi binafsi.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi, amevitaka vyama vya siasa kudumisha na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyao ili viweze kutekeleza majukumu yao kama taasisi imara.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amevikumbusha Vyama vya Siasa na Umma kwa ujumla kuhusu utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Gharama za uchaguzi.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa mafunzo maalumu kwa watumishi wa ofisi yake ili kuwajegea uwezo wa kufanya uangalizi wa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti 2018 katika jimbo la Buyungu na kata 79.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Mutungi amewaasa Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Vyama vya Siasa na Sheria za nchi kwa ujumla.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekutana na wajumbe wa Bodi za Wadhamini za Vyama vya Siasa katika kikao kilichofanyika leo siku ya Jumanne ya tarehe 29 Mei, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam.
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kimefanyika leo siku ya Alhamisi Mei 18, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Tume ya Kurekebisha Sheria Jijini Dara es salaam.