SUALA LA KUSIMAMIA VYAMA VYA SIASA LINAHITAJI UAMINIFU NA UADILIFU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Haruna Suleman amesema kuwa Suala la kusimamia vyama vya siasa nchini linahitaji umakini na usimamizi wa hali ya juu ikiwa ni njia bora ya kukuza democrasia na utawala bora nchini.
Hayo ameyabanishwa siku ya Ijumaa, Novemba 30, 2018 wakati akizungumza na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Mohammed Ally Ahmed aliyefika kwa mara ya kwanza Ofisini kwake Mazizini Mjini Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Jombe Magufuli mapema mwaka huu.
Mhe. Ahmed ambaye ameahidi ushirikiano na taasisi zote za Sheria nchini,pia ametumia fursa hiyo kukabidhi nakala ya Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa 2018 iliyosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni Dodoma, Novemba 16 mwaka huu kwa waziri huyo ambaye ni mojawapo wa wadau wa Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.