• English
  • Staff Mail
  • Maswali
  • Wasiliana Nasi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

  • Kuhusu sisi
    • Mamlaka
    • Dira
    • Majukumu
    • Muundo
    • Uongozi
    • Historia
  • Shughuli za Ofisi
    • Usajili wa Vyama
    • Uratibu wa Vyama
    • Ufuatiliaji wa Vyama
    • Gharama za Uchaguzi
    • Ruzuku ya Vyama
    • Utatuzi wa Migogoro
    • Taarifa za Vyama vya Siasa
  • Vyama vya Siasa
    • Usajili wa Kudumu
    • Usajili wa Muda
    • Orodha ya Vyama Vya Siasa
    • Baraza la Vyama
  • Sheria na Machapisho
    • Katiba
    • Sera
    • Sheria
    • Kanuni
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Fomu EE
    • Fomu PP
    • Fomu za Fedha
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Taarifa kwa Umma
  • Matangazo
    • Mikutano
    • Warsha
    • Nafasi za kazi
    • Zabuni
  • Ziara
    • Taratibu za Ziara
    • Fomu ya Maombi
    • Utimilifu na Makatazo
    • Maoni ya Watembeleaji

Serikali Yatoa Onyo kwa Vyama vya Siasa Vitakavyoshirikiana Kinyemela Wakati wa Kampeni

Na Mwandishi Wetu.

Vyama vya Siasa ambavyo vinatarajia kushirikiana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu bila kufuata Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyoainishwa kwenye Kifungu Na.11 (a) cha Sheria hiyo vitakuwa vimevunja sheria.

Onyo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, wakati alipofanya mahojiano kuhusu msimamo wa ofisi yake kwenye suala la ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Nyahoza amesema kuwa ushirikiano wa vyama hivyo umeratibiwa vizuri kisheria ambapo vyama vinapohitaji kushirikiana vinapaswa kutumia vikao halali vya chama badala ya utashi wa mtu binafsi. Msajili Msaidizi Nyahoza ameongeza kuwa baada ya vikao halali kupitisha azimio la kufanya ushirikiano vyama husika vinapaswa kuwasilisha mkataba wa ushirikiano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa miezi mitatu kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.

“Vyama havijakatazwa kushirikiana bali vimewekewa utaratibu ili Tume ya Uchaguzi pamoja na taasisi zote zinazohusika na uchaguzi ziweze kujiandaa vizuri na kuimarisha ulinzi hasa wakati wa kampeni pamoja na kuvisaidia vyama vingine kuelewa wanashindana na vyama vya aina gani” alisema Nyahoza.

Kuhusu ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 Msajili Msaidizi Nyahoza ameelezea kuwa mpaka sasa ofisi yake haijapokea mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kutoka kwa chama chochote cha siasa hivyo kwa mujibu wa sheriavyama ambavyo vina nia ya kushirikiana vimeshachelewa.

Aidha, Msajili Msaidizi Nyahoza amesema hadi sasa vyama vyenye usajili wa kudumu ni 19 na chama kimoja kina usajili wa muda na maombi ya vyama 16 bado yanafanyiwa upembuzi.

Habari

  • ZINGATIENI SHERIA, KATIBA NA KANUNI YA VYAMA VYENU - MUTUNGI.
    tokea mwezi 1
  • Political Parties Council Urges Ethical Campaigning, Applauds Government’s Gender Initiatives
    tokea miezi 3
  • Msajili Aipongeza CHADEMA kwa Kuonesha Ukomavu wa Demokrasia Nchini
    tokea miezi 5
  • Tanzia
    tokea miezi 6

Nifanyaje...

  • Kusajili Chama cha Siasa?

Machapisho

  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Msimamo wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya CHADEMA
  • KANUNI ZA KURATIBU MIKUTANO YA HADHARA YA VYAMA VYA SIASA YA MWAKA 2023
  • KANUNI ZA KURATIBU MIKUTANO YA HADHARA YA VYAMA VYA SIASA YA MWAKA 2023
  • THE POLITICAL PARTIES AFFAIRS LAWS (AMENDMENT) ACT, 2024
  • ORODHA YA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA 2025

Wasiliana Nasi

  • S.L.P : S.L.P 2851 Dodoma
  • Simu : +255 26 23322500
  • Nukushi : +255 26 2323525
  • Barua Pepe : info@orpp.go.tz
  • Website :https://www.orpp.go.tz

Kurasa za Karibu

  • eOffice
  • Video Mpya
  • Staff Mail
  • Huduma Zetu
  • Vyama Vya Siasa

Tovuti Mashuhuri

  • e-Mrejesho
  • Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Bunge la Tanzania
  • Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tume ya Uchaguzi

Mitandao ya Kijamii

© 2017 Office of Registrar of Political Parties - All Rights Reserved

  • Ramani Ya Tovuti
  • Sera YA Faragha
  • Angalizo