Majukumu
1. Kusajili vyama vya siasa na kuvifuta vile ambayo vimekiuka masharti ya usajili kw ujibu wa Sheria namba 5 ya mwaka 1992.
2. Kuratibu shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa
3. Kufuatilia mapato na matumizi ya vyama vya siasa katika uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010
4. Kufuatilia utendaji wa vyama vya siasa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992.
5. Kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa vyenye sifa
6. Kuwa kiungo kati ya Serikali na Vyama vya Siasa nchini
7. Kutoa elimu kwa umma kwa vyama vya siasa na wadau wa vyama vya siasa.