Baraza la Vyama vya Siasa
Baraza la Vyama vya Siasa limeundwa ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Wajumbe wa Baraza hili hujumuisha viongozi wa kitaifa wawili wa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndio yenye jukumu la kisheria ya kuratibu shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Makamu Mwenyekiti huchaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza.
Majukumu ya Baraza la Vyama vya Siasa
1. Kumshauri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya mgogoro inayotokea kwenye vyama vya siasa;
2. Kumsahuri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya masuala yenye maslahi kwa Taifa kuhusiana na vyama vya siasa au kuhusiana na hali ya kisiasa nchini;
3. Kuishauri Serikali kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya kupitishwa kwa marekebisho na utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria zingine zinazohusu masuala ya vyama vya siasa;
4. Kushauri juu ya kanuni zinazosimamia masuala yanayohusu vyama vya siasa;
5. Kutoa taarifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya uendeshaji wa chama chochote cha siasa.