Gharama za Uchaguzi
Ofisi husimamia utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 ambayo huratibu matumizi ya fedha wakati wa uteuzi, kampeni za uchaguzi na uchaguzi kwa lengo la kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za uchaguzi na kuweka uwanja sawa wa ushindani katika siasa
Utekelezaji wa Sheria hii hufanyika kwa kuhakikisha matakwa ya Sheria hii yanatekelezwa, kwa mfano, kuhakikisha wadau ( Wagombea Urais , Ubunge na Udiwani) wanapata fomu za gharama za uchaguzi na kuzijaza kwa wakati, kuhakikisha marejesho yanafanyika kwa wakati, kufuatilia mienendo ya wadau, wakati wa uteuzi, kampeni na uchaguzi ili kudhibiti vitendo vilivyokatazwa mfano rushwa , kushauri hatua za kuchukuliwa kwa ukiukwaji wa sheria hii .
Fomu za gharama za uchaguzi upatikana kwenye tovuti hii bonyeza hapa