• English
  • Staff Mail
  • Maswali
  • Wasiliana Nasi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

  • Kuhusu sisi
    • Mamlaka
    • Dira
    • Majukumu
    • Muundo
    • Uongozi
    • Historia
  • Shughuli za Ofisi
    • Usajili wa Vyama
    • Uratibu wa Vyama
    • Ufuatiliaji wa Vyama
    • Gharama za Uchaguzi
    • Ruzuku ya Vyama
    • Utatuzi wa Migogoro
    • Taarifa za Vyama vya Siasa
  • Vyama vya Siasa
    • Usajili wa Kudumu
    • Usajili wa Muda
    • Orodha ya Vyama Vya Siasa
    • Baraza la Vyama
  • Sheria na Machapisho
    • Katiba
    • Sera
    • Sheria
    • Kanuni
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Fomu EE
    • Fomu PP
    • Fomu za Fedha
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Taarifa kwa Umma
  • Matangazo
    • Mikutano
    • Warsha
    • Nafasi za kazi
    • Zabuni
  • Ziara
    • Taratibu za Ziara
    • Fomu ya Maombi
    • Utimilifu na Makatazo
    • Maoni ya Watembeleaji

WATUMISHI OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA WAPATIWA MAFUNZO UANGALIZI WA UCHAGUZI MDOGO.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa mafunzo maalumu kwa watumishi wa ofisi yake ili kuwajegea uwezo wa kufanya uangalizi wa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti 2018 katika jimbo la Buyungu na kata 79.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Julai 11, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa zikiwemo mada juu ya Elimu ya Maadili ya Vyama vya Siasa, Haki na wajibu wa Vyama vya Siasa, wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa, matendo yanayokatazwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa, Umuhimu wa kujaza fomu za gharama za Uchaguzi.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amewawataka watumishi hao kufanya kazi kwa ueledi na kwa kufuata sheria za nchi.

“ kila mmoja wetu atambue kuwa ofisi yetu imepewa dhamana kubwa ya kusimamia Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ili kudumisha demokrasia ya vyama vingi nchini, ni wajibu wetu kufanya kazi kwa ueledi na kwamujibu wa sheria” amesisitiza Jaji Mutungi

Naye Bi. Piencia C. Kiure mmoja wa wakufunzi katika mafunzo hayo ambaye ni Msajili Msaidizi anayeshughulika na masuala ya Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma amesisitiza umuhimu wa wagombea na vyama vya Siasa kurejesha fomu za Gharama za uchaguzi zinazobainisha mapato na maksio ya kiwango cha matumizi wakati wa uteuzi,kampeni na uchaguzi ndani ya mudauliotengwa kisheria ili kuepuka ukiukwaji wa sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Watumishi pia wamesisitizwa kuhakikisha wanavikumbusha vyama vya siasa na wagombea kunadi sera za vyama vyao kwa kusimamia maadili ya vyama vya siasa ili kuendelea kudumisha amani ya nchi.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni taasisi yenye wajibu wa kisheria wa kufanya uangalizi wa mwenendo wa chaguzi zinazofanyika kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wagombea na vyama vya siasa vinatekeleza matakwa ya sheria kwa kuepuka vitendo ambavyo vimekatazwa na sheria hizi ili kuimarisha demokrasia ya vyama vingi.

Habari

  • ZINGATIENI SHERIA, KATIBA NA KANUNI YA VYAMA VYENU - MUTUNGI.
    tokea mwezi 1
  • Political Parties Council Urges Ethical Campaigning, Applauds Government’s Gender Initiatives
    tokea miezi 3
  • Msajili Aipongeza CHADEMA kwa Kuonesha Ukomavu wa Demokrasia Nchini
    tokea miezi 5
  • Tanzia
    tokea miezi 6

Nifanyaje...

  • Kusajili Chama cha Siasa?

Machapisho

  • Taarifa kwa Umma Kuhusu Msimamo wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya CHADEMA
  • KANUNI ZA KURATIBU MIKUTANO YA HADHARA YA VYAMA VYA SIASA YA MWAKA 2023
  • KANUNI ZA KURATIBU MIKUTANO YA HADHARA YA VYAMA VYA SIASA YA MWAKA 2023
  • THE POLITICAL PARTIES AFFAIRS LAWS (AMENDMENT) ACT, 2024
  • ORODHA YA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA 2025

Wasiliana Nasi

  • S.L.P : S.L.P 2851 Dodoma
  • Simu : +255 26 23322500
  • Nukushi : +255 26 2323525
  • Barua Pepe : info@orpp.go.tz
  • Website :https://www.orpp.go.tz

Kurasa za Karibu

  • eOffice
  • Video Mpya
  • Staff Mail
  • Huduma Zetu
  • Vyama Vya Siasa

Tovuti Mashuhuri

  • e-Mrejesho
  • Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Bunge la Tanzania
  • Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tume ya Uchaguzi

Mitandao ya Kijamii

© 2017 Office of Registrar of Political Parties - All Rights Reserved

  • Ramani Ya Tovuti
  • Sera YA Faragha
  • Angalizo