WAZIRI WA NCHI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFUATA SHERIA ZA NCHI
Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa katika kudai haki katika masuala mbalimbali nchini ili kujiondoa katika matatizo yanayoweza kujitokeza na kuhatarisha amani ya nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, (Sera, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama wakati akitoa ufafanuzi juu ya hoja za wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ziliyojitokeza wakati wa kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti 2017/2018 na makadirio ya bajeti ya mwaka 2018/2019 ya mafungu ya taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo Ofisi ya Msajii wa Vyama vya Siasa nchini, Leo Machi 28,2018 katika ukumbi wa mikutano Bungeni Dodoma.
“Kila raia anatakiwa kufuata na kutekeleza matakwa ya sheriana taratibu zilizowekwa na nchi ili kujiondoa katika matatizo ambayo yanayoweza kujitokeza kutokana na ukiukwaji wa sheria, tujenge tabia ya utii wa sheria bila shuruti” amesisitiza Mhe Mgahama
Wakati wa majadiliano ilibainika kuwa vipo baadhi ya vyama vya siasa ambayo vimeonyesha kwa wazi kabisa vikiwa katika hali ya kuvilazimisha vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za kisheria na kisha vyama hivyo hivyo hurudi kuilaumu Serikali.
Aidha, Mhagama amefafanua kuwa hoja zilizohusisha mgogoro wa ruzuku na uongozi wa Chama cha Wananchi CUF, maandamano, migogoro ya vyama vya siasa na hoja zote ambazo kuna kesi makahamani, kuachwa bila kujadiliwa kwa kuwa kuzijadili hoja hizo kunaweza kuharibu mwenendo wa kesi.
Mhe. Mhagama ametoa wito kwa vyama vyote nchinikufuata utaratibu wa mahakamawa kukata rufaa endapo vitaona haki haijatendeka .
Ikumbukwe siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeshindwa kufuata sheria na taratibu za nchi na kupelekea vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani, kitendo ambacho kimepelekea matendo ya uvunjifu wa amani.