BARAZA LA WAFANYAKAZI LAKUTANA
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kimefanyika leo siku ya Alhamisi Mei 18, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Tume ya Kurekebisha Sheria Jijini Dara es salaam.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji .Francis Mutungi amewataka wajumbe kushiriki kikamilifu bila hofu kwa kutumia fursa hiyo muhimu kujadili hoja zinazojitokeza ili kufanikisha shughuli za Taasisi.
Katika kufikia malengo ya kikao hicho, wajumbe wamepata fursa ya mafunzo nakujadili mada ya Mapitio ya Bajeti ya ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka 2018/2019, Sheria ya mifuko ya hifadhi ya Jamii yam waka 2017 na fursa za uwezeshaji.
Baraza la Wafanyakazi ni Baraza ambalo lipo kwa mujibu wa Agizo la Rais Na. 1 la mwaka 1970 ambalo lina lengo la kuwashirikisha wafanyakazi wa ngazi zote katika utekelezaji wa shughuli za Taasisi kwa kushirikiana na Uongozi.