KAMATI YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI YAMSHAURI MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUMALIZA MGOGOGO WA CUF

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeishauri Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kuchukua jitihada za kutosha kusuluhisha migogoro katika Chama cha Wananchi CUF ili kuepusha athari kubwa zinazoweza kujitokeza katika Muungano.
Ushauri huo umetolewa April 4, 2018 Mjini Dodoma wakati Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, akitoa maoni ya kamati yake kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2017/2018 na makadirio ya Mapato na Matumizi ya mwaka 2018/2019 ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake ikiwemo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa