Vyama vya Siasa ambavyo vinatarajia kushirikiana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu bila kufuata Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyoainishwa kwenye Kifungu Na.11 (a) cha Sheria hiyo vitakuwa vimevunja sheria. Soma zaidi..
Karibu kwenye tovuti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa . Kupitia tovuti hii, utapata taarifa za uhakika juu ya shughuli za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na taarifa za uhakika juu ya Vyama vya Siasa.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imejikita katika usimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 ili kuhakikisha uwepo na ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini.
Vyama vya Siasa ambavyo vinatarajia kushirikiana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu bila kufuata Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyoainishwa kwenye Kifungu Na.11 (a) cha Sheria hiyo vitakuwa vimevunja sheria. Soma zaidi..
Serikali inawaonya Wanasiasa kuacha propaganda za kupindisha ukweli na kutoa tafsiri potofu kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2018 kwa lengo la kuuhadaa umma kukataa muswada bali watumie fursa hii baada ya kuusoma , kutoa maoni yao stahiki kwa lengo la kuuboresha Soma zaidi..
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi anawataarifu wajumbe wote wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa kikao cha Baraza la Vyama vya siasa kilichokuwa kimepangwa kufanyika tarehe 21 na 22 Desemba, 2018 mjini Zanzibar, kimeahirishwa. Soma zaidi..
Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kimefanyika leo Disemba 4, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. Soma zaidi..