Jaji Mutungi afanya mazungumzo na IGP Wambura
02 Feb, 2026
Msajili wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi amefanya mazungumzo ya kikazi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camilius Wambura leo Tarehe 02 February, 2026 katika Ofisi ya IGP jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yalikuwa ya kawaida na yalifanyika katika muktadha wa ushirikiano wa kitaasisi kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi, kwa lengo la kuimarisha mawasiliano na uratibu wa utekelezaji wa majukumu ya kila taasisi kwa mujibu wa sheria.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaendela kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za serikali kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa, vyama vya siasa na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi nchini.