Wasifu

Mhe. Jaji
Francis S. K. Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa
NENO LA UKARIBISHO
Nawakaribisha kwa moyo wa dhati kwenye tovuti rasmi ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Tovuti hii ni sehemu mahsusi ya mawasiliano baina ya ofisi yetu, Vyama vya Siasa, wadau wa demokrasia, na wananchi wote.
Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ina jukumu la kusimamia usajili wa Vyama vya Siasa, kufuatilia uendeshaji wake, na kuhakikisha kuwa vinafanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, sheria, na maadili ya kisiasa. Kupitia tovuti hii, tunalenga kuonesha uwazi katika utendaji kazi wetu na kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa wakati na kwa urahisi.
Tovuti hii imebeba nyaraka, miongozo, taarifa za usajili, shughuli za elimu ya uraia kwa umma na taarifa nyingine muhimu zitakazowasaidia wadau wote kupata uelewa mpana kuhusu mfumo wa vyama vya siasa nchini. Tunaamini kuwa upatikanaji wa taarifa sahihi ni nguzo muhimu ya kujenga jamii inayoshiriki kikamilifu katika masuala ya kisiasa kwa njia ya amani na uwajibikaji.
Tunawaalika watu wote muendelea kutumia tovuti hii kama chanzo rasmi cha maarifa na taarifa, na pia kutoa maoni au maswali yatakayosaidia kuboresha huduma zetu.
Karibuni sana.