JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Jaji Francis Mutungi akutana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa katika Umoja wa Afrika(UNOAU) Bw. Parfait Onanga-Anyanga
10 Mar, 2026
Jaji Francis Mutungi akutana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa katika Umoja wa Afrika(UNOAU) Bw. Parfait Onanga-Anyanga

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji(Mstaafu) Francis Mutungi, leo jijini Dar es Salaam, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa katika Umoja wa Afrika(UNOAU) Bw. Parfait Onanga-Anyanga. Kwenye mazungumzo yake na mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu, Jaji Mutungi alimweleza hatua mbalimbali ambazo ofisi yake ilizichukua kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa na mazingira bora ya demokrasia ya vyama vingi.