Nifanyaje...
Kuna hatua mbili katika kusajili chama cha siasa kwa kufuata mashart yafuatayo;
i. Usajili wa Muda
Kunatakiwa Waanzilishi wawili watakaowasilisha kwa Msajili wa Vyama vya vya siasa maombi ya usajili wa muda kwa kujaza fomu maalumu wakiambatanisha na katiba na kanuni za chama kinachotarajiwa.
Maombi yataambatana na kulipa ada ya maombi ya usajili ya shilingi 25,000.
Usajili wa muda utadumu kwa muda wa siku 180, ndani ya muda huo, chama kitatakiwa kutafuta wanachama wasiopungua 200 katika mikoa 10, mikoa miwili kati ya hiyo ni lazima iwe Tanzania Zanzibar na mkoa mmoja kati ya hiyo miwili, uwe Pemba.
ii.Usajili wa Kudumu
Baada ya kupata wanachama 200 ndani ya siku 180 (Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itafanya uhakiki kujiridhisha), Chama kinatakiwa kuwa na usajili wa muda na chama kiwe;
kimechagua viongozi wa Kifaifa na kiwe kina Ofisi ya Makao makuu na anuani ya posta kwa ajili ya mawasiliano rasmi.
Baada ya kutiiza mashart yaliyoorodheshwa, Waanzilishi watawasilisha maombi ya usajili wa kudumu kwa kujaza fomu maalumu. Maombi ya usajili wa kudumu yataambatana na kulipa ada ya usajili wa kudumu ya shilingi 50,000