Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Francis Mutungi akizungumza na washiriki wakati wa mafunzo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa yaliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, leo tarehe 18 Agosti 2025.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, akiambatana na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mohamed Ali Ahmed, leo jijini Dar es Salaam amekutana na Mwenyekiti wa Misheni ya Awali ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SEAC,mheshimiwa Jennifer Chiriga.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis S. K. Mutungi atembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba leo tarehe 5 Julai 2025 jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa (RPP), Mhe. Jaji Francis Mutungi akifungua Mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) uliofanyika leo tarehe 2 Juni, 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Multifunctional – Confusious
Baadhi ya watumishi wa ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa wakiendelea na zoezi la uhakiki katika ofisi ndogo ya chama cha TLP kilichopo kata ya Fuoni wilaya ya Magharibi B,Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar tarehe 21 Mei 2025.
Katika picha ni watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiongozwa na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Ndg. Sisty Nyahoza, pamoja na viongozi wa Chama cha ADC mara baada ya kumaliza Zoezi la Uhakiki katika ofisi ndogo za ADC Zanzibar.
Watumishi wa Kitengo cha TEHAMA wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakijadili jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Ndg. Masoud Ali Abdallah, mjadala huo ulikuwa ni sehemu ya zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi ndogo ya chama hicho.
Mwezeshaji wa mada kuhusu Sera ya usawa wa kijinsia kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la WiLDAF, Dkt. Deus Kibamba akiwasilisha mada wakati wa siku ya pili ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kilichofanyika leo tarehe 15 Mei, 2025 mjini Morogoro.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Dkt. Emmanuel Mkilia (kushoto) kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa tarehe 14 Mei,2025 mjini Morogoro
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Ndg. Mohammed Ali Ahmed akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya viongozi wa vyama vya siasa leo tarehe 6 Mei, 2025 yaliokuwa yakifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dar es Salaam.