TANZIA
29 Dec, 2025
TANZIA
Mhe. Msajili wa Vyama vya Siasa anasikitika kutangaza kifo cha Ndg. CPA. Mbogo Alexander Munubi, aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, aliyefariki ghafla mkoani Dodoma, leo tarehe 28 Disemba 2025.
Mipango ya mazishi inaratibiwa na familia ya Marehemu ikishirikiana na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Taarifa rasmi na ratiba ya mazishi zitatolewa kadri maandalizi yanavyokamilika.
Msajili wa Vyama vya Siasa anatoa pole kwa watumishi wote, familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu. Mungu awafariji wote katika kipindi hiki kigumu, tuendelee kumuombea Marehemu apumzike kwa amani.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mbogo Alexander Munubi mahali pema peponi, Amina.