Msajili wa Vyama vya Siasa Atengua Uteuzi wa Wagombea Urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani wa Chama cha ADC na ACT Wazalendo kwa kukiuka kanuni
27 Aug, 2025

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, ametengua uteuzi wa wagombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa udhamini wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) na Alliance for Democratic Change (ADC). Abaini ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba na Kanuni za vyama vyao.
Ametumia fursa hiyo kuviasa vyama vya siasa vyenye usajili kamili kuzingatia sheria za nchi, kudumisha demokrasia, amani, utulivu na umoja wa kitaifa wakati huu na baada ya uchaguzi.
#nyumbayademokrasia
#achaseraziongee