Tanzia
Msajili wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi, anasikitika kutangaza kifo cha Bwana John Bill Tendwa, aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuanzia mwaka 2001 hadi 2013. Mheshimiwa Tendwa amefariki dunia leo, tarehe 17 Desemba 2024, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa na familia kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Kibamba Hospitali.
Ratiba na taarifa rasmi za mazishi zitatolewa mara baada ya kukamilika.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi.