MKUTANO WA WADAU WATAJWA KUWA DHAMIRA NAMBARI MOJA KUFIKIA MUFAKA WA KITAIFA
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mkutano uliowakutanisha Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya siasa nchini umetajwa kama kitendo ambacho ni dhamira namba moja inayoonyesha kuna lengo Madhubuti la kufika muafaka wa kitaifa kwa maslahi mapana ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Jaji Francis Mutungi leo tarehe 7 Septemba, 2025 i Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serana wakati wa Mkutano waKitaifa wa Wadau Kutafakari Hali ya Kisiasa nchini, Uchaguzi Mkuu wa 2025 na Mustakabari wa Taifa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Serena Hotel.
“Mimi nataka kuwasihi kitendo cha kukutana hapa ni dhamira nambari moja kuonyesha tunalengo Madhubuti la kufikia muafaka fulani kwa maslahi mapana ya taifa letu” alisisitiza Jaji Mutungi
Aidha ametoa rai kwa washiriki wa Mkutano huo kujikita kwenye hoja zitakazopelekea kupatikana kwa majawabu ya nini kinapaswa kufanyika badala ya kuzua mabishano, mivutano ambayo mwisho wake hali inayoweza kupelekea kutofikiwa kwa lengo mahususi la Mkutano huo.
“Wengine tutakao kuwa tunazungumza au kuzungumzwa tuwe na moyo wa kupokea,kusikiliza tuwe na moyo wa usikivu tusianze kunyoosheana vidole kwamba Prof. Tibaijuka ndiye muhusika? Hapana, nilitaka kutambu uwepo wako kwa sababu nimekuana ndiyo unaingia” Amesema Jaji Mutungi.
Amesisitiza kuwa kuwa lengo na madhumuni ya mkutano huo si kunyooshea vidole kwani kwa kufanya hivyo hakuna kitakachofanikiwa kwani kwa kufanya hivyo mkutano huo hautakuwa na manufaa yoyote kwa maslahi mapana ya taifa letu.
Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) nakuwakutanissha viongozi wa vyama vya siasa wanaounda TCD na vyama waalikwa ambavyo siyo wajumbe wa kituo hiko TCD ni asasi ya kiraia inayoundwa na Vyama vya Siasa ambavyo vinaakuwa na wawakilishi bungeni ambapo kwa sasa inaundwa na CCM, CHAUMMA, ACT Wazalendo na NCCR Mageuzi. Wadau wengine walioshiriki ni wazee wastaafu,, asasi za kiraia.wawakilishi wa mashirikia ya kimataifa na viongozi wa dini.