JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUENDELEZA CHACHU YA UMOJA WA KITAIFA
03 Sep, 2026
BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUENDELEZA CHACHU YA  UMOJA WA KITAIFA

Na: Mwandishi Wetu -ORPP

Baraza la Vyama vya Siasa limejipanga kuendelea kuwa chombo muhimu kitakachotumika kuwaunganisha wananchi ili kudumisha umoja mshikamano na amani iliyopo nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Mhe. Juma Ali Khatibu wakati wa Kikao cha Baraza hilo cha kilichofanyika leo tarehe 3 Septemba 2026 katika Ukumbi wa Mikutano Morogogoro Hotel mjini Morogoro.

“ Tumeshuhudia mambo mengi yamepita tumemaliza uchaguzi na sasa Serikali inakwenda mbele na kazi zinafanyika kwa hiyo sisi sasa tunakwenda kuwaunganisha wananchi poamoja na wanasiasa kwa kuhubiri amani” alisema Khatib.

Ameongeza kuwa baraza hilo litakuwa na wajibu wa kuhakikisha wanasiasa wanaungnishwa na wananchi ili kuleta amani mongoni mwa jamii hali itakayopelekea wanchi kuendelea na shughuli zao za kujipatia ridhi.

Aidha ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wanasiasa kutambua wajibu wao wa kutangaza sera za vyama vyao kwa maslahi mapana ya vyama vyao na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Naibu Msajili wa Vyama Vya Siasa, Mh. Mohammed Ali Ahmed amesema kuwa uundwaji wa Baraza la Vyama vya Siasa umekamilika rasmi leo baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Kamati za Kisekta za Baraza hilo.

Kama hizo ni pamoja na Kamati ya Maadili na Mahusiano, Kamati ya Sheria na Utawala Bora, Kamati ya Masuala ya Uchaguzi na Kamati ya Bunge na Siasa.

Amesema kuwa kwa  mujibu wa Kanuni za Baraza la Vyama vya Siasa baraza hili ltahudumu kwa kipindi cha miaka miwili mingine ijayo ambapo utaitishwa uchaguzi kwa ajili ya kuwachagua viongozi wapya.

“ Tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka miwili kupata viongozi wapya kwa mujibu wa demokrasia ya vyama vya siasa” amesema Naibu Msajili.

Aidha ametoa pongezi kwa wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi  na kuongeza kuwa sambamba na suala zima la uchaguzi, wajumbe  wamepata fursa ya kupata mafunzo kuhusu hifadhi ya jamii iliyotolewa na wataalamu kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii kwa Sekta Binafsi (NSSF).

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Baraza la Vyama vya Siasa amabaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara amesema kuwa Baraza la Vyama vya Sias ani chombo muhimu katika kuleta utengamano na ujenzi wa  taifa sambamba na demokrasia.

Amesema kuwa katika uongozi wao ambao umechaguliwa wataakikisha suala zima la mchakato wa maridhiano ya kitaifa linapewa kipaumbele ili kujange umoja na mshikamano na taifa letu.

“Na hasa mimi nikiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, hatua kubwa tutakayokuja kuiangalia hapo mbele sisi Kamati ya Uongozi ni pamoja na masuala ya maridhiano ya kitaifa kujenga umoja wa taifa letu la Tanzania” Alisisitiza Majalio.

Amesema kuwa ni Imani yake kwamba katika umoja kuna maendeleo na kila Mtanzania anahitaji maendeleo kwa ajili ya taifa na maendeleo ya kila mmoja mmoja na kubainisha kuwa hay oni miongoni mwa majukumu yao ambapo wataka na kushauriana, kujadiliana na kuishauri Serikali kwa yale watakayokubaliana kwa pamoja kama Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania.

Kikao hiki kimefanyika ikiwa ni ukamilishaji wa mchakato wa upatikanaji wa viongozi wapya wa Baraza hilo ambao ukaa katika nafasi zao kwa kipindi cha miaka miwili ambapo awali ulitanguliwa na uchaguzi wa kuwapata Mwenyekiti wa Baraza na Makamu wake ambaye hata hivyo nafasi yake ilibaki wazi kufuatia mabadiliko na hivyo pamoja na uchaguzi wa viongozi wa Kamati za kisekta kikao hiki kilichagua na kumthibitisha  Makamu mpya wa Baraza hilo ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Agrey Mwanri.

slot gacor