BARAZA LA VYAMA VYA SIASA LAJA NA MKAKATI KUONGEZA UFANISI
Na: Mwandishi Wetu, ORPP
Baraza la Vyama vya Siasa limeafiki kutoa pongezi za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameendelea kuimarisha Demokrasia nchini kwa kuboresha Baraza la Vyama vya Siasa nchini.
Hayo yamebainishwa na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Kamati ya Uongozi ya Braza la Siasa ambaye Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Ndg. Salum Mwalimu wakati akitoa salaam kwa niaba ya Baraza hilo kabla ya uchaguzi wa viongozi wapya wa Kamati ya Uongozi ya baraza hilo uliofanyika leo tarehe 24 April 2024 Zanzibar katika Ukumbi wa Spring Hall Madinat Al Bahr Hotel leo.
“ Kuna wakati tumemuweka Jaji Mutungi kwenye kitimoto lakini ni wahakikishie tuendelee kuweka imani kwenye kamati ya uongozi, mtakumbuka hatukuwa na Bajeti kwenye Baraza la Vyama vya Siasa lakini chini ya kamati yenu tumefanyakazi kubwa sana mpaka leo msije mkasema na mpigia mtu kampeni lakini ndani ya miaka miwili tuna bajeti yetu iliyopitishwa Bungeni,na tumeandaa mikutano miwili mikubwa ambayo imeleta tija kubwa kwa Taifa letu, yote haya ni nia njema ya Serikali kuhakikisha Demokrasia inazidi kuimarika” Alisema Salum Mwalimu.
Aliongeza kuwa kuundwa kwa Kikosi kazi ni zao la Baraza la Vyama vya Siasa kilichotokana na Baraza hili kupitia Kamati ya Uongozi na Sekretarieti chini ya Jaji Francis Mutungi na tumefanikiwa kuandaa mikutano miwili ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Bara na Visiwani.
“Mheshimiwa Jaji amesema kabla ya kikao cha Baraza kutakuwa na vikao vya Kamati jambo ambalo tumelipigania muda mrefu sana hii inaonyesha Dhahiri nia njema ya Serikali kuhakikisha Demokrasia inaimarika, mtaona kwa mara ya kwanza juzi kuna kadude kameingia kwenye vyama vyetu kuhakikisha tunasafisha karoti na kuhakikisha akaunti ipo active, kazi ile imefanywa kwa wivu mkubwa na kamati ya uongozi na kupokelewa na Jaji Mutungi na Sekretairieti na wakaitekeleza ndani ya muda mfupi, na mheshimiwa Jaji kuna jambo alilisema ambalo kilikuwa kilio chetu cha muda mrefu cha kamati kukakaa kabla ya Baraza” aliongeza Mwalimu.
Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi alisema kuwa wakati wanapanga mikutano ya Baraza la Vyama vya Siasa vitatanguliwa na vikao vya Kamati za Baraza la Vyama vya Sias ambavyo vipo kikanuni kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
“Ebu tulionyeshe Taifa ili kuwa tuliopo hapa tuna haki yakukutana na kujadiliana, jana nilitakakusema kwamba Kamati ya uongozi haiwezi kukaa kabla Kamati hazijakaa, kiutaratibu zinatakiwa zile kamati kukaa arafu wenyeviti wanakuja kutuambia yaliyojiri kutoka katika kamati zao” Ailisema Jaji Mutungi.
Jaji Mutungi aliongeza kuwa lengo la kuwa na vikao vya kamati kabla ya kikao cha Baraza ni kuhakikisha kuwa masuala yote yanayojadiliwa katika Baraza yawe yametoka chini kwenyevyama husika ikiw...