JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

VYAMA VYA SIASA VYOTE NI SAWA HAKUNA CHAMA KIDOGO WALA KIKUBWA
12 Aug, 2026
VYAMA VYA SIASA VYOTE NI SAWA HAKUNA CHAMA KIDOGO WALA KIKUBWA

Vyama vya Siasa vyote nchini vina hadhi sawa na hakuna chama kinachopaswa kujiona chenyewe ni kikubwa kiliko vingine kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Palamagamba J. A. Kabudi alipokuwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyam,a vya Siasa wakati wa  ziara yake ya  kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa linalojengwa katika eneo la Kilimani jijini Dodoma leo tarehe 11 Agosti, 2026.

“Hakuna chama ambacho kimepewa haki chache wala wajibu mdogo ndani ya Katiba, vyama vyote vina hadhi sawa, viko sawa kwahiyo si sahihi na wala si hekima na wala haiendani na sheria kusema sisi n chama cha aina hii nah awa ni vyama vidogo” Alisisitiza Profesa Kabudi

Profesa Kabudi  aliongeza kuwa hakuna vya vidogo vyama vyote vipo saw ana vina jukumu linalofanana na kazi yao kubwa ya kwanza ni ushawishi wa kisiasa kwa wananchi ili wafuate sera zao kwa ajili ya maendeleo ya taifa na maslahi mapana ya taifa sambamba na ulinzi na usalama wa taifa.

Katika hatua nyingine Waziri Kabudi ameipongeza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi lenye hadhi stahiki ya unyeti wa Ofisi ya Msajili na kutaka ujenzi ukamilike haraka ili Ofisi iweze kuhamia katika jengo hilo.

Amesema kuwa jengo hilo lina hadhi na litajitosheleza katika kuhudumia wadau wa siasa na demokrasia ya vyama vingi nchini ikiwemo Baraza la Vyama vya Saisa kwa uwepo wa kumbi na ofisi kwa ajili ya matumizi ya baraza hilo ambo ndicho chombo cha kuunganisha vyama vyote nchini.

Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mstaafu Francis Mutungi amesema kuwa Ofisi ilifikia uamuzi wa kujenga jengo hilo kwa mtazamo wa miaka mingi ijayo ambapo Ofisi itahitaji kuwa na wataalam mbalimbali wakiwemo wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wataalam wa elimu ya jamii,watafiti

Jaji Mutungi ameongeza kuwa Jengo hilo litakuwa Kitovu cha Demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki na kusini mwa bara la Afrika ambapo watu watakuja kujifunza masuala ya siasa nchini kwetu

na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mstaafu Fransis Mutungi  amemshukuru Waziri kwa maelekezo aliyotoa, ambapo amesema mipango ya ofisi ni kuwa na watendaji wenye elimu ya siasa, wataalamu wa elimu jamii ambao watasaidi kuchakata na kutoa muongozo kulingana na mambo yanavyokwenda. Akaongezea kwa kusema,

"Taasisi hii ni kitovu cha mambo ya siasa tunahitaji wataalamu wenye ujuzi tofauti watakaosaidia katika kufanya tafiti na kutoa taarifa zenye weledi zitakazosaidia taasisi kufanya kazi vizuri zaidi,"

Akiwasilisha taarifa fupi kuhusu mafanikio ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ndg, Magohu Zonzo amesema kuwa ujenzi wa Ofisi hii unatekelezwa na alisema kuwa mradi huu unatekelezwa na Kampuni ya Group Six International kwa gharama ya shilingi bilioni 20,431,828,643.50 ambapo mpaka sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 90 kwa kazi ya ujenzi wa jengo nae neo la nje na asilimia 65 kwa kazi za mifumo ya umeme na mitambo.

slot gacor