JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Profesa Kabudi Kuzindua Baraza la Sita la Vyama vya Siasa. Wadau wa demokrasia kushikiriki.
06 Oct, 2026
Profesa Kabudi Kuzindua Baraza la Sita la Vyama vya Siasa. Wadau wa demokrasia kushikiriki.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la Sita la Vyama vya Siasa, itakayofanyika tarehe 7 Oktoba 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mount Meru, Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo inatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa demokrasia ya vyama vingi katika kipindi ambacho Tanzania inaendelea kuimarisha mfumo wa siasa za vyama vingi na kuendeleza mazungumzo yanayojenga uelewano na ushirikiano miongoni mwa vyama vya siasa.

Katika kuendeleza juhudi hizo, Baraza la Vyama vya Siasa linatoa nafasi kwa viongozi wa vyama kushirikiana na kushauriana kuhusu masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi na hali ya kisiasa nchini. Baraza hilo limeanzishwa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258.

slot gacor