Jaji Mutungi afanya mazungumzo na Mhe. Lazarus Chakwera, Rais wa Zamani wa Malawi na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.
14 Apr, 2026
Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Mstaafu Francis Mutungi amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Lazarus Chakwera, Rais wa Zamani wa Malawi na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola. Kikao hicho ni sehemu ya ziara ya Mhe. Chakwera nchini ambapo anakutana na makundi mbalimbali ya wanasiasa, taasisi na viongozi wa Serikali.Kikao hicho kimefanyika tarehe 10 April, 2026 katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zilizopo Mtaa wa Shaban Robert Jijini Dar es Salaam.