OFISI YA MSAJILI VYAMA VYA SIASA YAPONGEZWA UENDESHAJI ZOEZI LA UHAKIKI WA VYAMA VYA SIASA
Na: Frank Shija, ORPP
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imepongezwa kwa namna ambavyo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Vyama vya Siasa vinajiendesha kama taasisi na kwa kuzingatia sheria na taraatibu za kidemokrasia.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Ndg. Doyo Hassan Doyo wakati akitoa shukrani mbele ya wawakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa walipofika katika Ofisi za Makao Makuu ya ADC zilizopo Ilala, Buguruni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa vyana vya siasa mapema karibu
“Wengine tunapata elimu kupitia dodoso hizi hata katika uendeshaji masuala yetu binafsi mbali na shughuli za chama hivyo zoezi hili limekuwa msaada mkubwa sana kwetu hali inayofanya tuendelee kuwajibika kama mnavyoona”, alisema Doyo.
Doyo aliongeza kuwa kutokana na elimu wanayoipata kupitia zoezi la uhakiki inaonyesha Dhahiri kwamba vyama vya siasa vinatakiwa kuongeza ufanisi zaidi kiatika namna ya kujiendesha kama taasisi ya umma ambapo gharama zinahitajika katika kufanikisha hilo.
“Menejimenti kuiendesha ni gharama hili bado tunasisitiza wenzetu mlione kama Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu mgao wa ruzuku kwa Vyama vya siasa muangalie namna ya kutubusti nadhani mnaona namna ambavyo tunajiendesha kwa matatizo kama haya ya kudaiwa kodi” alisisitiza Doyo.
Hata hivyo amesema kuwa sisi kama chama tumenufaika pakubwa sana kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutokana na viongozi wetu mbalimbali kujengewa uwezo kupitia semina mbalimbali zilizoandaliwa na Ofisi ya Msajili.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Muhidin Mapeyo ametoa pongezi hizo kwa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kwa namna ambavyo wamejitahidi kurekebisha pale ambapo mapungufu yalibainika wakati wa zoezi la uhakiki lililopita.
“ Vitu vingi ambavyo tulikuwa tunavihitji vimefanywa na tena kwa ubora na ubora uliokuwa unahitajika, kwa hiyo nimpongeze sana Katibu Mkuu kwa mgawanyo wa majukumu pongezi hizi pia zimfikie Mwenyekiti wa chama kwa kazi nzuri mnayoifanya” alisema Mapeyo.
Mapeyo aliongeza kuwa zoezi la uhkaiki limekuwa na tija sana kwa ustawi wa Vyama vya Siasa kwani kupitia zoezi hili vyama vya siasa vimezidi kuimarika hali inayopelekea hata kuongezeka kwa ufanisi katika namna ya utunzaji wa hesabu zao na kupelekea kupungua kwa hati chafu za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaendelea na zoezi la ukakiki wa vyama vya siasa nchinilililoanza tarehe 29 April 2014 jijini Dar es Salaam ambapo linahusisha Ofisi za Makao Makuu ya Vyama vyote kwa Pnade zote mbili za Muungano kwa maana ya Tanzania Bara na Zanzibar na linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 28 Mei 2024 jijini Dodoma, mpaka sasa jumla ya vyama nane vimekwisha hakikiwa am...