Malengo

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ina malengo yafuatayo:-

  1. Kuhakikisha Vyama vya Siasa vinafanya shughuli za kisiasa kwa kuzingatia Sheria za nchi;
  2. Kuhakikisha Demokrasia ya vyama vingi vya siasa inaimarika;
  3. Wananchi wanakuwa na uelewa mzuri wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na matakwa ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi;
  4. Wananchi wanachagua viongozi wao kwa kuzingatia sifa na kukubalika kwa mgombea na sio rushwa ya aina yoyote ile;
  5. Kudumisha amani, utulivu na mshikamano uliopo katika nchi yetu, kwa kuhakikisha Vyama vya Siasa vinafanya shughuli za kisiasa bila kuhatarisha amani, utulivu na mshikamano uliopo katika nchi yetu.
 
 
Follow Us: